Yeye ni rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuhudhuria mkutano huu tangu alipohudhuria Bill Clinton mwaka 2000.
Wachambuzi wanasema wajumbe wengi wanaohudhuria wanatarajiwa kukinzana juu ya maoni yenye ushindani ya mustakbali wa uchumi wa dunia.
Trump anategemewa kusukuma ajenda yake ya “Marekani Kwanza,” ambayo imeshuhudia Marekani ikiweka tozo katika baadhi bidhaa zinazoingizwa na kudai kufanyike mabadiliko ya makubaliano ya biashara za kimataifa.
Mataifa mengine yenye nguvu duniani, zikiwemo nchi za Ulaya , China na Japan, zinasisitiza kuwepo makubaliano mapya juu ya uhuru wa biashara za kimataifa.
Wanaoandaa mkutano huu wanatarajia kuwa itatoa fursa ya kutafuta muwafaka juu ya malengo mbalimbali yanayokinzana.