Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:40

Trump aeleza ajenda za utawala wake


Rais Donald Trump atoa hotuba kwenye kikao cha pamoja cha bunge la Marekani.
Rais Donald Trump atoa hotuba kwenye kikao cha pamoja cha bunge la Marekani.

Rais Donald Trump amelaani uhalifu na vitisho vya karibuni vilivyolenga vituo vya wayahudi na ubomoaji wa makaburi yao.

Wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mbele ya wajumbe wa Congress kwenye mkutano wa pamoja Jumanne usiku, amesisitiza kuwa uvunjaji uliofanywa kwenye makaburi ya wayahudi “unatukumbusha kwamba sisi ni nchi ambayo inasimama ikiwa imeungana pamoja na kulaani vikali aina zote za chuki.”

Rais Donald Trump amesema Marekani itaendelea na vita dhidi ya kile alichokiita ‘Ugaidi wa Kiislamu,’ na kusema kuwa utawala wake utashirikiana na mataifa ya Kiislamu duniani kuwaangamiza magaidi duniani kote.

Amesema utawala wake utatumia dola trilioni moja na kusema kuwa atalihimiza bunge kuidhinisha matumizi yatakayoimarisha jeshi la Marekani. Aidha, Trump ameahidi kukata kodi kwa watu wa kiwango cha kati lakini hakutoa maelezo yoyote kuhusu jinsi atakavyogharamia program hiyo.

Trump Speech
Trump Speech

Trump alitoa hotuba yake ya kwanza ya ‘hali ya kitaifa’ kwa wabunge na wageni waalikwa huko, huku makamu rais Mike Pence na spika wa bunge Paul Ryan wakiwa wamesimama nyuma yake.

Trump Speech
Trump Speech

“Tunachokishuhudia hivi leo ni kufufua upya imani ya wamarekani, ambapo washirika watagundua kwamba marekani kwa mara nyingine imekuwa kiongozi,” alisema rais Trump.

XS
SM
MD
LG