Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 14:59

Trump asitisha safari za Boeing 737 Max 8 na Max 9 Marekani


Rais wa Marekani Donald Trump, Jumatano jioni alitangaza amri ya dharura ya kusitisha usafiri wa ndege zote muundo wa Boeing 737 Max 8 na Max 9, kwenye anga ya Marekani.

Hii, Trump alisema, ni hadi pale uchunguzi utakapokamilika kubaini iwapo hitilafu ya kimitambo ilisababisha ajali mbili za Ndege aina ya Max 8, katika kipindi cha chini ya miezi mitano, na kupelekea vifo vya mamia ya watu.

Muda mfupi baada ya Trump kutangaza hatua hiyo, maafisa wakuu wa kampuni ya Boeing inayotengeneza Ndege hizo, walitoa taarifa kupitia mtandao wa Twitter na kusema kwamba kapunmi hiyo inaunga mkono kauli ya rais huyo na kuongeza kwamba "ni heri kuwa salama kuliko kujuta baadaye."

Marekani sasa imejiunga na takriban nchi 30 ambazo tayari zimetangaza kusitishwa kwa safari za Ndege hizo huku uchunguzi wa mfumo wake wa kompyuta, ambao unashukiwa kusabisha ajali ya ndge hiyo mwezi Oktoba mwaka jana nchini Indonesia, na ile ya ndege ya shirika la Ethiopian Airlines, Jumapili iliyopita, ukiendelea.

Hatua ya Marekani ya AJumatano ni kinyume na na msimamo wa awali, uliokuwa umechukuliwa na mamlaka ya safari za Angani ya Marekani, FAA, ambayo Jumanne ilitangaza kwamba haikuwa na mipango ya kusitisha safari za Ndege aina ya Boeing 737 Max 8, iliyogubikwa na mzozo tangu ajali ya Jumapili iliyotokea karibu na mji mkiuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kuua watu wote 157 waliokuwemo.

Katika amri yake, Trump amezitaka Ndege zote za muundo wa Max 8 na Max 9 ambazo zilikuwa angani wakati wa tangazo hilo, ziegeshwe punde tu zitakapotua.

"Marubani wote wamefahamishwa hilo pamoja na Mashirika yote ya ndege," alisema Trump.

Licha ya FAA na mashirika ya ndege ya Marekani kukaa kimya kufuatia shinikizo za kutaka ndege hizo zisitishae safari zake, wachambuzi wa masuala ya teknolojia ya ndege wanasema kuna uwezekano mkubwa wa hitilafu za kiuhandisi hasa kwenye mfumo wa kompyuta kwa ndege hizo za 737 Max.

Kufikia Jumapili ambapo ajali ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikielekea mjini Nairobi ilitokea, Boeing ilikuwa imeuza ndge 400 ulimwenguni kote.

Wachambuzi wanasema kuwa hili ni pigo kubwa kibiashara, kwa kampuni ya Boeing na mashirika mbalimbali ya Ndege ulimwenguni kote.

XS
SM
MD
LG