Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:27

Trump atangaza Heather atachukuwa nafasi ya Nikki Haley


Balozi Nikki Haley
Balozi Nikki Haley

Rais Donald Trump ametangaza Ijumaa anamchagua msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Heather Nauert kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa (UN).

“Ni mwanamke mwenye kipaji, hodari, mwepesi na nafikiri ataheshimiwa na watu wote,” Trump amesema Ijumaa kabla ya kuondoka White House akielekea Jiji la Kansas, Missouri kikazi.

Iwapo atapitishwa na Baraza la Seneti, Nauert, mwandishi wa habari wa kituo cha Fox News ambaye alikuwa na uzoefu mdogo wa sera ya mambo ya nje kabla ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, atachukuwa nafasi iliyoachwa na Nikki Haley.

Haley, gavana wa zamani wa South Carolina, alitangaza Octoba kuwa ataachia nafasi hiyo ifikapo mwisho wa mwaka huu. Nauert atakuwa ni sauti ya mstari wa mbele ya Trump juu ya sera za kigeni za Marekani.

​
XS
SM
MD
LG