Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:48

Marekani kuendeleza vikwazo dhidi ya Sudan Kusini


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley.

Msemaji wa Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema Jumanne kwamba Juba huenda ikafanya mashauriano na serikali ya Marekani juu ya vikwazo ambavyo vimewekwa hivi karibuni kwa watu watatu wakiwemo maafisa wawili waandamizi wa Sudan Kusini.

Balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa, Nikki Haley hata hivyo ametetea vikwazo hivyo alipozungumza kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani na kulitaka baraza hilo kuchukua hatua.

“Marekani haisubiri hatua. Mapema mwezi huu, tumeweka vikwazo vya kiuchumi na kifedha dhidi ya watu binafsi ambao waliingilia kati utaratibu wa amani, na kuzuia fursa za misaada ya kibinadamu na kuingilia kati tume ya ulinzi wa Amani”. Marekani itafanya kila iwezalo kupunguza madhila nchini Sudan Kusini na baraza la usalama na watendaji wa kieneo lazima wafanye mengi zaidi alisema Haley. Aliliambia baraza la usalama kuwa Marekani ina ujumbe mzito kwa viongozi wa Sudani Kusini.

XS
SM
MD
LG