Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:05

Trump asema usalama mashuleni 'kipaumbele chetu'


Usiku wa maombolezo ya mauaji ya Florida
Usiku wa maombolezo ya mauaji ya Florida

Mtu anayedaiwa kuwa na matatizo mwenye umri wa miaka 19 anayetuhumiwa kuuwa watu 17 huko katika shule mmoja ya Florida ameshikiliwa bila ya dhamana.

Nikolas Cruz alifikishwa kwa muda mfupi mahakamani kusomea mashtaka yake 17 ya kuuwa kwa kukusudia.

Kufikishwa kwake mahakamani kumekuja masaa kadhaa baada ya Rais Donald Trump kutoa hotuba fupi katika ikulu ya White House kufuatia janga hilo la mauaji, akisema atakutana kwa haraka na maafisa kutoka nchi nzima kutafuta ufumbuzi juu ya suala la maradhi ya akili ili kuzuia mauaji ya watu wengi na kufanya usalama mashuleni “ ni kipaumbele chetu.”

Hakutaja jambo lolote kuhusu pendekezo la kudhibiti silaha nchini.

Lakini sheria za udhibiti wa silaha zilikuwa katika fikra za watu wengi waliohudhuria usiku wa maombolezo ya wahanga wa mauaji ya shule ya sekondari ya Stoneman Douglas huko mjini Parkland, Florida.

XS
SM
MD
LG