Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 20:41

Mauaji ya Florida yamerudisha mjadala wa kumiliki silaha Marekani


Mfyatuaji risasi Nikolas Cruz (C) akisimama mahakamani kwa mara ya kwanza

Wanafunzi, wazazi, waalimu na wanasiasa ni miongoni mwa watu waliokua wakitoa matamshi makali siku ya Alhamisi dhidi ya ghasia za bunduki na kutaka sheria ya mageuzi ya kumiliki bunduki zipitishwe kufuatia mauwaji ya watu 17 katika shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Douglas yaliyotokea katika jimbo la Florida siku ya Jumatano.

Wito mpya kwenye mtandao uliopewa jina la #Gunreformnow unaendelea kua suala kuu kwenye mitandao ya kijamii na kuvuma ambapo wa-Marekani wengi wanatoa wito wa kupunguzwa biashara ya bunduki na utumiaji wa bunduki kubwa za kivita ambazo kawaida hutumika katika matukio mengi ya mauwaji ya halaiki nchini Marekani.

Nikolas Cruz, mfyatuaji risasi kwenye shule huko Florida
Nikolas Cruz, mfyatuaji risasi kwenye shule huko Florida

Mshambuliaji wa mauwaji hayo Nikolas Cruz, mwenye miaka 19 inasemekana ni kijana mwenye matatizo ya kiakili alifunguliwa rasmi mashtaka 17 mbele ya mahakama ya Florida siku ya Alhamisi.

Hakimu Kim Theresa Mollica aliamrisha kijana huyo ashikiliwe bila ya kupewa dhamana na alimuambia Cruz “una mashtaka ya uhalifu mbaya.”

Kufikishwa kwake mahakamani kumetokea muda mfupi baada ya Rais Donald Trump kuhutubia taifa na kuamrisha bendera zote kufungwa nusu mlingoti kwa siku moja ili kuomboleza tukio la mauaji yaliyotokea katika shule hiyo ya sekondari huko Florida.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG