Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:58

Trump asema tawala dhalimu hazina maisha marefu


Watu wakiandamana karibu na Chuo Kikuu cha Tehran
Watu wakiandamana karibu na Chuo Kikuu cha Tehran

Rais wa Marekani Donald Trump Trump, amesema utawala wa mataifa yanayokandamiza raia hayana maisha marefu, akizungumzia maandamano yaliyofanyika nchini Iran.

Trump ameeleza kuwa iko siku itafikia ambapo raia wa Iran watafanya maamuzi.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesisitiza kuwa uvunjifu wa amani wowote utakabiliwa kwa nguvu zote. Wizara hiyo imepuuzia mbali tamko la Trump alilolituma katika akuanti yake ya Tweeter.

Waziri Abdolrahman Rahmani Fazli, amewataka wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani kuacha mara moja vitendo vya uharibifu wa mali za umma na kuwaonya kuwa sheria itachukua mkondo wake.

Mitandao ya jamii ilionyesha picha za video ambapo waandamanaji wawili walipigwa risasi katika mji wa Dorud- Magharibi mwa taifa hilo.

Katika eneo la Ab-har, Kaskazini mwa nchi hiyo, waandamanaji waliteketeza picha ya kiongozi wa kiroho nchini humo Ayatollah Ali Khamenei.

Huko katika mji wa kihistoria wa Mashhad gari na pikipiki za jeshi la polisi zilichomwa moto na waandamanaji.

Wakati huo huo katika Jiji la Teh-ran, maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika uwanja mmoja wa mikutano, wakitoa wito kwa jeshi na polisi kuungana nao.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC maeneo mengi ya mji mkuu, polisi na makundi ya kiusalama yenye silaha, hayakuonekana kabisa.

Awali, maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono utawala wa nchi hiyo walikuwa na mkutano wao pia.

XS
SM
MD
LG