Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 18:45

Trump asema Kim Jong Un anafursa ya kufanya linalostahili


Kim Jong Un

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuna “nafasi nzuri” ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un atatenda “linalostahili kwa watu wake na kwa binadamu” kwa kuchukua hatua ya kupunguza silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Katika ujumbe wa Twitter ulioonekana Jumatano, Trump amesema anangojea kwa hamu mkutano alioupanga wa kukutana na Kim lakini amesisitiza haja ya kuendeleza “vikwazo na shinikizo kubwa” kwa wakati huu.

China imesema wakati wa ziara ya siri ya Kim huko Beijing, alithibitisha kuwa ana nia ya dhati kupunguza silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea na kushiriki katika mazungumzo yatakayo zishirikisha Marekani na Korea Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya China, Xinhua, Kim alifanya ziara hiyo ambayo haikuwa rasmi kuanzia Jumapili mpaka Jumatano na kukutana na Rais Xi Jinping.

Trump amesema Xi amemtumia ujumbe akisema mkutano wake na Kim ulikwenda vizuri na kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini anahamu ya kukutana na Trump.

Katika ujumbe wake mwengine, Trump alikuwa anaelezea jinsi atakavyo lishughulikia suala la Korea Kaskazini

Katika tukio hili la kukutana Kim-Xi, Msemaji wa White House Sarah Sanders amesema Jumatano kuwa White House inaeleza kwa tahadhari matumaini yake, na inahisi “kuwa mambo yanaonyesha muelekeo mzuri,” akiongeza kuwa mkutano kati ya Kim na Xi ni “dalili nzuri kwamba shinikizo hilo kubwa lililofanyika limeonyesha kufanya kazi.”

Sanders ameeleza kuwa ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Kim nje ya nchi tangu achukue uongozi wa Korea Kaskazini, na White House inachukulia hilo kuwa ni “alama nyingine nzuri kuwa shinikizo hilo kubwa linafanya kazi.”

Iwapo mkutano huo utaendelea kufanyika mwezi May, Sanders amewaambia waandishi kuwa White House inataka kuhakikisha “unafanyika kwa haraka tutavyoweza,” lakini “tunataka kuhakikisha kuwa unafanyika vizuri, na tunajitayarisha kwa kufanikisha lengo hilo.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG