Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:20

Matamshi ya Trump kwenye video yazua mtafaruku wa kisiasa


Mgombea kiti cha rais wa Republican Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wake wa kisiasa Oct 4 2016.
Mgombea kiti cha rais wa Republican Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wake wa kisiasa Oct 4 2016.

Spika wa bunge la Marekani, Paul Ryan, Ijumaa usiku alikuwa mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa chama cha Republikan, kuelezea kutamaushwa kwake na matamshi aliyoyatoa mgombea wa kiti cha rais wa chama chama hicho, Donald Trump, ambayo pia yametajwa na Wamarekani wengi kama ya matusi ya kudhalilisha wanawake.

Hii ilikuwa ni kufuatia kuibuka kwa video iliyo na sauti yake akijivunia namna alivyomfuata mwanamke mmoja akijaribu kua pamoja nae lakini alishindwa, akitumia maneno ya matusi.

Trump alikiri kutamka maneno yaliyotaja sehemu za siri za mwanamke kwa njia ya kudhalilisha alipokua anazungumza na mtangazaji wa kipindi cha televisheni 'Access Hollywood,' akiwa anafahamu mazungumzo yao yanarikodiwa hapo mwaka 2005.

Video hiyo inamuonyesha mwanasiasa huyo, ambaye siku hizo alikuwa mfanyabiashara na msanii, akizungumza na ripota wa makala hayo ya "Access Hollywood," Billy Bush, ambaye ni binamu wa aliyekuwa rais wa Marekani George W Bush.

"Nililtaka kulala na mwanamke huyo hata ingawa alikuwa ameolewa. Nilimpeleka kununua samani na nilitaka kufanya mapenzi naye lakini nikashindwa," Trump anasikika akisema kwenye kanda hiyo. "Mimi huvutiwa sana na wanawake warembo. Na kwa sababu ya hadhi, mtu anaweza kufanya chochote nao...hata kama ni kuwavuta kwa sehemu za siri....na wanapendelea sana," alisema.

Baadaye alionekana akitoka kwenye basi hilo na kumpa mkono mwanamke mwingine ambaye alikuwa amemsema kwa njia ya kudhalilisha.

Siku ya Ijumaa, Trump aliomba msamaha kupitia ujumbe wa Twitter, na baadaye usiku akatoa video akielezea kwamba alifanya makosa.

Punde baada ya video hiyo kuchapishwa na gazeti la Washington Post, Trump aliandika kauli ifuatayo kwenye mtandao huo wa kijamii: "Naomba msamaha iwapo nilimuudhi yeyote. Lakini Bill Clinton ameshawahi kusema mambo mabaya kuliko hayo tulipokuwa tukicheza golf."

Baada ya video hiyo kuchezwa na vyombo vingi vya habari Marekani kote na kuzua mjadala mkubwa, Trump alirekodi na kutuma video yake kwa vyombo vya habari na kukubali kwa kauli moja kwamba alifanya makosa na kwamba ameomba msamaha. "Maishani mwangu nimefanya na nimesema mambo yasiyoridhisha, na huu ni mmoja wa wakati huo."

Ijumaa usiku shirika la habari la CNN liliripoti kuwa Spika Ryan, ambaye alikuwa aandamane na Trump katika kampeni kwenye jimbo la Wisconsin siku ya Jumamosi, alisikitishwa mno na maneno ya mgombea huyo, na kusema kuwa hakutaka mgombea huyo kuhudhuria mkutano huo.

Baadaye, mgombea mwenza wa Trump, Mike Pence, ambaye alikuwa amealikwa kwa mkutano huo,alitangaza kwamba hatahudhuria.

Haya yalijiri siku mbili tu kabla ya mdahalo wa pili wa wagombea urais siku ya Jumapili, ambao umetajwa na wachambuzi wa maswala ya kisiasa kama muhimu mno kuelekea kwa uchaguzi utakaofanyika Novemba 8 mwaka huu.

XS
SM
MD
LG