Akiulizwa ikiwa anaweza kugombea tena katika miaka minne ijayo iwapo hatafanikiwa katika kuwania kiti cha urais kwa mara ya tatu mfululizo, rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 78 alimwambia mwandishi wa habari wa Marekani Sharyl Attkisson: “Sidhani. Sidhani kwamba hilo litatokea. Sidhani kabisa. Tunatumai tutafanikiwa.”
Trump anakabiliwa na ushindani mkubwa dhidi ya mshindani wa chama cha Democrat Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, huku kura ya maoni ikionyesha ushindani mkali kati ya wagombea hao wawili katika majimbo ambayo yanaamua mshindi wa uchaguzi, licha ya kuwa Harris anaonekana kuongoza katika kura ya maoni kwenye ngazi ya taifa.
Forum