Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 15:09

Trump akutana na viongozi wa juu wa Republican katika bunge


Mitch McConnell, kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti Marekani.
Mitch McConnell, kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti Marekani.

Warepublican katika baraza la seneti wanaonekana kukubaliana na ukweli uliofikiriwa ni miujiza kwamba mfanyabiashara bilionea wa New York, Donald Trump ni mgombea rais mtarajiwa katika chama chao.

Trump alishinda uteuzi kwa njia ya kizamani inayotumika kwa kupata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote alisema kiongozi wa walio wengi katika seneti, Mitch McConnell Jumanne baada ya miezi kadhaa ya kukataa kuto maoni yake juu ya mchakato wa kinyang’anyiro cha urais.

Alisema “tunaheshimu sauti za wapiga kura wa Republican katika uchaguzi wa awali kote nchini”. Trump anatarajiwa kukutana na wabunge wa Republican katika mabaraza yote mawili siku ya Alhamis, atakutana ana kwa ana na baadhi yao ambao wameelezea kutomuunga mkono katika harakati zake za kuwania uteuzi, ikimjumuisha spika wa bunge Paul Ryan ambaye amekataa kumuidhinisha Trump.

XS
SM
MD
LG