Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:38

Trump anakanusha ripoti ya kutounga mkono uwepo uchunguzi zaidi kwa wamiliki bunduki


Rais wa Marekani Donald Trump akiwa katika moja ya mjadala wa kumiliki bunduki Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa katika moja ya mjadala wa kumiliki bunduki Marekani

Trump alisema anataka bunduki kuwa mikononi mwa watu ambao hawana matatizo ya akili na anataka watu hao waweze kupata bunduki kiurahisi. Lakini kwa watu ambao ni wagonjwa, hataki wawe na fursa ya kupata bunduki

Rais Donald Trump anakanusha ripoti aliyomwambia mkuu wa chama kinacholinda haki ya raia kumiliki bunduki nchini Marekani-NRA kwamba kuongeza historia ya uchunguzi kwa wanunuzi wa bunduki sio moja ya masuala ya kujadiliwa na hivi sasa anasema anaunga mkono hatua hiyo ya kuongeza uchunguzi kwa wanunuaji wa bunduki.

Rais Trump alizungumza na waandishi wa habari nje ya White House siku ya Jumatano wakati akielezea namna anavyopanga kuhutubia ghasia za bunduki nchini Marekani. Alisema anafikiria njia za kuboresha zaidi uchunguzi kwa wanunuaji bunduki lakini alionya kile anachoita kuwa wazo ambalo kwa kiasi fulani haliendani na kipengele cha pili cha katiba ya Marekani, anaamini kwamba itadhibiti umiliki halali wa bunduki.

Rais wa marekani, Donald Trump
Rais wa marekani, Donald Trump

Trump aliongeza kuwa anataka bunduki kuwa mikononi mwa watu ambao hawana matatizo ya akili na anataka watu hao waweze kupata bunduki kiurahisi. Lakini kwa watu ambao ni wagonjwa, hataki wawe na fursa ya kupata bunduki.

Mjadala kuhusu kuwepo ukaguzi zaidi kwa wanunuzi wa bunduki umerudi tena baada ya watu wawili wenye silaha walipofanya matukio ya mauaji kwa ufyatuaji risasi holela kwenye mji wa El Paso katika jimbo la Texas na pia katika mji wa Dayton kwenye jimbo la Ohio na kusababisha vifo vya watu 31 mwanzoni mwa mwezi huu nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG