Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:06

Trump ana imani Kim Jong Un yuko tayari 'kufikia amani'


Mtu anapita mbele ya bango linalo onyesha picha ya Rais Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Tokyo, Japan Machi 9, 2018.
Mtu anapita mbele ya bango linalo onyesha picha ya Rais Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Tokyo, Japan Machi 9, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumamosi kwamba anaamini kuwa Korea Kaskazini iko tayari “kufikia amani” baada ya kiongozi wake Kim Jong Un kutangaza kuwa yuko tayari kukutana na rais wa Marekani.

“Nafikiri wakati umewadia,” Trump amesema katika mkutano wa kisiasa katika eneo la kuegesha ndege huko mji wa Moon, Jimbo la Pennsylvania.

Kim ni “mtu aliyesambaza silaha za nyuklia kila mahali,” lakini hivi sasa “hatorusha tena makombora hewani” wakati mpango uko njiani wa mkutano wa ana kwa ana ambao ni wakipekee kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na Marekani, Trump amesema.

Ameongeza kuwa wakati atakapokutana na Kim, “ Inawezekana nikaacha mkutano kwa haraka au tunaweza kukaa pamoja naye na kufikia makubaliano ya kipekee kwa manufaa ya dunia.”

Trump amedai kuwa ni juhudi zake zilizowezesha michezo ya Olympic ya kipindi cha baridi kufanikiwa ambayo iliandaliwa na Korea Kusini hivi karibuni, akiongeza kuwa bila ya juhudi zake za kudhibiti tishio la shambulizi la nyuklia, michezo hiyo “isingefanikiwa kabisa.”

XS
SM
MD
LG