White house imesema rais Donald Trump Marekani amekubali ukaribisho wa Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un wa kutaka wakutane lakini imesema kuwa vikwazo vyote dhidi ya Korea Kaskazini vitaendelea kuwepo.
Kim ameeleza azma yake ya kukutana na Trump kupitia mshauri wake wa usalama Chung Eui yong Chung ambaye alitoa tangazo hilo la kihistoria alhamisi usiku nje ya white house.
Msemaji wa White house Sarah Huckabee Sanders ameandika katika ukurasa wake wa tweeter kwamba Trump na Kim huenda wakakutana kwa muda na sehemu itakayokubaliwa.
Chung kwa muda mfupi alitokea nje ya white house mbele ya waandishi wa habari na kusema kwamba “Kim ana hamu kubwa ya kukutana na Trump haraka iwezekanavyo” pia ameongeza kwamba Kim ana nia ya dhati ya kuachana na silaha za nyuklia na majaribio ya makombora hayo.