Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:40

Trump amteua mkosoaji mkuu wa 'Obamacare' kuwa waziri wa Afya


Mbunge kutoka jimbo la Georgia, Tom Price, aliyeteuliwa na rais mteule Donald Trump kuwa waziri wa Afya.
Mbunge kutoka jimbo la Georgia, Tom Price, aliyeteuliwa na rais mteule Donald Trump kuwa waziri wa Afya.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump Jumanne alimteua mbunge kutoka jimbo la Georgia, Tom Price, aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa mpango wa huduma za afya mashuhuri ya utawala wa rais Barack Obama, kuwa waziri wa Afya na huduma za jamii.

Wakati wa kampeni yake, Trump aliahidi kuwa angeondoa bima ya afya maarufu Obamacare lakini baada ya ushindi wake, amesema kuwa kuna baadhi ya sehemu za bima hiyo anazofikiri zinafaa kudumishwa.

Aidha, siku ya Jumatatu, Trump alikutana na mjumbe mwingine mwenye uwezekano wa kuwa waziri wa mambo ya nje na aliekuwa mkuu wa idara ya ujasusi ya CIA generali David Petreus ingawa anatarajiwa kuibua maswali makali kwenye braza la senate. Petreus alikuwa kamanda mkuu nchini Iraq na pia aliongoza vikosi vya NATO nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG