Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 17:35

Trump amfukuza Bannon White House


 Steve Bannon
Steve Bannon

Rais wa Marekani Donald Trump Ijumaa amewaambia maafisa wa ngazi ya juu ameamua kumfukuza mshauri wa sera, Steve Bannon.

Bannon ambaye kuanzia mwanzo wa miezi sita ya malumbano ya kiuongozi amekuwa ni katika washauri wake Trump ambaye ana utata mkubwa kuliko wote.

Bannon, ambaye amepewa sifa ya kumsaidia Trump kuingia madarakani, alikuwa na migongano kwa miezi kadhaa na watu wengine ambao ni wenye sauti katika ofisi ya West Wing ya ikulu.

Mkuu wa wafanyakazi wa White House John Kelly na Steve Bannon walikubaliana kuwa Ijumaa iwe siku ya mwisho kwa Bannon kutumikia wadhifa wake huo.

Msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders amesema White House inamshukuru Bannon kwa utumishi wake.

Bannon kwa mujibu wa gazeti la The New York Times amesisitiza kwamba kuondoka kwake ilikuwa ni chaguo lake, na alikuwa amepeleka barua ya kujiuzulu kwa rais siku 11 zilizopita ili itangazwe rasmi kuanzia wiki hii.

XS
SM
MD
LG