Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:45

Trump awakashifu viongozi wa Republican wasiomuunga mkono


Mgombea urais wa Republican, Donald Trump
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump

Mgombea urais Marekani m-Republican Donald Trump siku ya Jumanne aliwakashifu wa-republican wenziwe kwa kutomuunga mkono kwenye kampeni yake ya kuingia White House na badala yake wanalenga kwenye kinyang’anyiro cha wabunge na baraza la wawakilishi ili chama kiendelee kudhibiti bunge lijalo.

Wakati huo huo mgombea urais wa Democratic, Hillary Clinton anafurahia kuongoza kwa pointi kadhaa dhidi ya mpinzani wake na wataalamu wanampatia asilimia 88 ya fursa ya kushinda uchaguzi mkuu huku baadhi ya warepublican wenye vyeo vya juu wakikiri ushindi kwa nafasi ya urais unakwenda kwa Democratic.

Spika wa bunge la Marekani, Paul Ryan.
Spika wa bunge la Marekani, Paul Ryan.

Trump aliwakaripia baadhi ya warepublican wasiomuunga mkono kupitia mtandao wa Twitter akimuita spika wa bunge la Marekani, Paul Ryan kuwa ni kiongozi mwenye mapungufu na asiye na mwelekeo kutokana na kutangaza kwake hatompigia tena kampeni bwana Trump.

XS
SM
MD
LG