Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:33

Trump amemteuwa mkwewe kama mshauri wa rais


Jared Kushner, mkwe wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump
Jared Kushner, mkwe wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump

Vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba Jared Kushner, mkwe wa rais mteule wa Marekani atateuliwa kuwa mshauri mwandamizi wa rais.

Maafisa waliopo katika kipindi cha mpito walithipitisha taarifa hizi kwa vituo vya televisheni cha NBC na CNN vya Marekani. Rais mteule Donald Trump, alipoulizwa Jumatatu kuhusu jukumu la Kushner katika utawala wake alisema “tutazungumzia hilo siku ya Jumatano”. Siku ambayo rais mteule wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 amemuoa mtoto wa kike wa Trump, Ivanka Trump.

XS
SM
MD
LG