Trump alisema jeshi linajua, na kwamba kuna jambo la ajabu linaendelea, akiwaambia waandishi wa habari akiwa Mar-a-Lago, Florida katika mkutano wake wa kwanza na wanahabari toka achaguliwe kwa muhula mpya wa miaka minne unaoanza mwakani.
Baada ya Trump kuzungumza, Meja Jenerali wa jeshi la anga Pat Ryder, msemaji wa Pentagon, aliwaambia wanabari kwamba hakuna ushahidi kwa sasa kwamba kuonekana huko kwa ndege zisizo na rubani ni tishio la usalama wa taifa, umma, au kuwa kuna kuingiliwa na mataifa ya kigeni.
Forum