Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:22

Rais Trump akutana na Papa Vatican


Papa akutana na Rais Donald Trump na Mkewe Melania
Papa akutana na Rais Donald Trump na Mkewe Melania

Rais Donald Trump na Papa Francis wamefanya mkutano wa dakika 30 huko Vatican Jumatano.

Viongozi hawa wawili wamesisitiza umuhimu wa dini hizi tatu (Ukristo, Uislamu na Uyahudi) zinazoshirikiana katika kuwa na kiongozi mmoja ambaye ni Mtume Abraham (Ibrahim) katika ziara yake ya kwanza akiwa rais nchi za nje.

Viongozi hao wawili wakikutana kwa mara ya kwanza, walipeana mikono. Papa alionekana akiwa mkimya. Wakati rais alikuwa akitabasamu.

“Ni heshima kubwa kukutana na wewe,” Trump alisema kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani baada wote kuketi katika chumba maalum cha kujisomea cha Papa.

Baada ya rais kuwa na mkutano wa faragha na Papa katika Jumba Takatifu kulikuwa na muda mfupi kwa watu wengine katika ujumbe wa msafara wa Marekani kukutana naye.

Wale waliokuwepo katika ujumbe huo walikuwa ni Mke wa Trump, Melania, Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson, Mshauri wa Usalama wa Taifa H.R. McMaster, Mtoto wa Kike wa Trump, Ivanka na mumewe Jared Kushner (ambao hivi sasa ni washauri rasmi wa rais).

Katika kukutana kwao pia walibadilishana zawadi.

“Hii ni zawadi yako. Hivi ni vitabu kutoka kwa Martin Luther King. Nafikiri utavifurahia sana,” rais alimwambia Papa.

Papa alimpa Trump medali iliyotengenezwa na mwanasanaa wa Roma. Alisema ni tawi la mzeituni ambalo ni alama ya amani.

“Tunaweza kutumika amani,” rais alijibu.

“Hivi naweka saini yangu mwenye katika sanaa hii kwa ajili yako,” Papa alimwambia Trump.

XS
SM
MD
LG