Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 19:38

Trump akanusha kutoa tamko la kudhalilisha


Rais Donald Trump amekanusha kuwa alitumia neno lenye kudhalilisha katika kuzielezea nchi za Kiafrika na Haiti wakati wa mkutano wake Ikulu ya White House.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti Alhamisi kuwa Trump alitumia kauli hiyo katika mazungumzo juu ya sera ya uhamiaji ya Marekani inayojulikana kama DACA.

DACA ni progamu ya kuchelewesha kuchukuliwa hatua kwa watoto walioingia nchini (DACA). Ilikuwa inawakusudia watu ambao walihamia Marekani kinyume cha sheria kabla hawajafikia umri wa miaka 16.

Chini ya sera hiyo, wahamiaji hao wanapewa utetezi na hawawezi kuondolewa nchini.

Ripoti za vyombo vya habari Marekani zimesema kuwa Trump alitumia maneno ya kashfa wakati maseneta Dick Durbin na Lindsey Graham walipomueleza kuhusu muswada mpya ulioandikwa wa wahamiaji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG