Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 03:13

Trump akana hana hatia kwa mashtaka dhidi yake yanayohusiana na uchaguzi wa 2020


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Ronald Reagan, kabla ya kuelekea mahakamani kusikiliza mashtaka dhidi yake, Agosti 3, 2024.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Ronald Reagan, kabla ya kuelekea mahakamani kusikiliza mashtaka dhidi yake, Agosti 3, 2024.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Alhamisi amekana hana hatia kwa mashtaka kwamba alipanga njama ya kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020 ambao alishindwa.

Waendesha mashtaka walikitaja kitendo hicho kuwa juhudi ambazo hazijawahi kushuhudiwa za rais huyo wa zamani kudhoofisha misingi ya demokrasia.

Mwendesha mashtaka maalum Jack Smith, ambaye alisimamia uchunguzi wa serikali kuu, alikuwepo mahakamani wakati Trump anavyojitetea mbele ya jaji Moxila Upadhyaya.

“Sina hatia, Trump amesema, akisisitiza neno la kwanza.

Kesi hiyo ilidumu kwa nusu saa, ilifanyika katika mahakama ya Washington, umbali wa kilomita 1 kutoka jengo la Bunge la Marekani lililoshambuliwa na wafuasi wa Trump tarehe 6 Januari mwaka 2021, ili kujaribu kulizuia Bunge kurasimisha kushindwa kwa Trump katika uchaguzi wa 2020.

Ilikuwa mara ya tatu Trump akijitetea kuwa hana hatia tangu mwezi Aprili, huku kukitarajiwa miezi kadhaa ya malumbano ya kisheria kabla ya kesi kuanza kusikilizwa rasmi, mchakato ambao utagongana na kampeni za urais ambapo Trump ndiye mshindani aliye mbele katika uchaguzi wa awali kuwania uteuzi kuwa mgombea wa chama cha Republican atakayeshindana na Rais Mdemocrat Joe Biden.

Forum

XS
SM
MD
LG