Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:26

Trump aikosoa Canada kwa "utovu wa urari wa kibiashara"


Rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau .
Rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau .

Rais wa Marekani Donald Trump na waziri wa biashara Wilbur Ross, walisema Jumanne kwamba hawana hofu na vita ya kibiashara na Canada, baada ya maamuzi ya Marekani kuiathibu katika biashara ya maziwa na mbao.

Trump alisema Canada haina urari mzuri wa biashara na Marekani, na kuongeza kusema watu hawatambui hilo na nchi hiyo jirani imekuwa ikiitendea Marekani vibaya kwa kuwazidi mbinu wanasiasa wa Marekani kwa miaka mingi.

Trump aliongeza kwamba anataka kuona bidhaa za Canada zikiwekewa kodi kubwa hasa za mbao na miti.

Alitoa kauli hiyo katika mkutano na wakulima wa Marekani ambapo alitia saini amri ya utendaji kuhusiana na kilimo na maeneo ya mashambani.

Sarafu ya Canada ilishuka thamani kufikia kiwango cha chini katika kipindi cha kwa miezi 14 baada ya Marekani kuweka ushuru wa awali wenye wastani wa asilimia 20, ikiwa ni zaidi ya dola bilioni katika ushuru wa mbao laini za Canada.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amepinga tuhuma hizo za Truimp na kusema Canada italinda kwa nguvu maslahi ya kiwanda cha mbao cha Canada.

XS
SM
MD
LG