Maoni hayo yamekuja siku moja baada ya Trump kusema kutakuwa na Jehanamu kwao ikiwa Hamas haitawaachilia mateka waliosalia wanaoshikiliwa huko Gaza.
“Waachilie Mateka wote sasa, sio baadaye, na mrudishe mara moja miili ya watu mliowauwa, au ni mwisho wenu" Trump alisema kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social.
"Ninatumia Israeli kila kitu inachohitaji ili kumaliza kazi, hakuna hata mwanachama mmoja wa Hamas atakuwa salama ikiwa hamtafanya kama ninavyosema," Trump aliongeza.
Awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano ilimalizika Jumamosi iliyopita. Ilijumuisha Hamas kuwaachilia huru mateka 33, watano raia wa Thailand, na Israel iwaachilie wafungwa 2,000 wa Palestina.
White House ilithibitisha Jumatano kuwa imewasiliana moja kwa moja na Hamas. Vyanzo vinavyofahamu suala hilo wamesema mazungumzo yalilenga kuachiliwa kwa mateka wa Marekani ambao bado wanashikiliwa huko Gaza.
Msemaji wa White House Karoline Leavitt alielezea mazungumzo hayo kama juhudi zenye nia njema za kufanya kilicho sahihi kwa watu wa Marekani.
Afisi ya waziri mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu ilitoa taarifa ikisema kuwa Israel imeielezea Marekani msimamo wake kuhusu mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas.
Forum