Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 03:28

Trump aendelea kuwa gumzo kwenye mdahalo wa pili


Mgombea urais wa Republican anayeongoza Donald Trump (L), na Gavana wa zamani wa jimbo la Florida, Jeb Bush, katika mdahalo wa pili huko Simi Valley, Sept. 16, 2015.

Mgombea urais wa Republican anayeongoza, bilionea Donald Trump alishiriki kwenye mdahalo wa pili wa chama chake Jumatano usiku katika kinyang’anyiro cha kwania uteuzi akikabiliwa na shutuma kwamba hafai kuwa rais ajaye.

Wagombea 10 waliungana na bilionea huyo kwenye mdahalo mkali uliofanyika kwenye jengo la maktaba ya Rais Ronald Reagan huko Simi Valley, katika jimbo la California. Bwana Trump alielezea uzoefu wake kama mfanyabiashara ili kuwapa changamoto wapinzani wake.

Alisema ana mtazamo wa kipekee na rekodi katika biashara ambayo itamsaidia ulimwenguni. Pia alisema ataelewana na viongozi wa dunia akiwemo Rais wa Russia, Vladimir Putin.

Wagombea urais wa Republican, Ben Carson (L) na Donald Trump
Wagombea urais wa Republican, Ben Carson (L) na Donald Trump

Mazungumzo ya bwana Trump kuipingaWashington, pamoja na madai ya kuwafukuza wahamiaji haramu milioni 11 kutoka Marekani na kuwabeza wapinzani wake kumepelekea yeye kuwa juu katika ukusanyaji maoni uliofanywa kwa wapiga kura wa Republican. Ukusanyaji maoni wa CBS/New York Times wiki hii ulimuonyesha bwana Trump akiwa na asilimia 27 ya uungwaji mkono, akimzidi kidogo mgombea mwingine aliyekuwa na asilimia 23, mtaalamu wa zamani wa upasuaji, Dr. Ben Carson.

Hakuna wagombea wengine waliokuwepo kwenye jukwaa katika mdahalo wa Jumatano ambao wamepata uungwaji mkono wa tarakimu mbili zaidi ya Trump na Carson.

Katika suala la mkataba wa nyuklia wa Iran, Seneta wa jimbo la Kentucky, Rand Paul na Gavana wa zamani wa jimbo la Florida, Jeb Bush walisema rais ajaye anatakiwa haraka kuubadili mkataba huo.

XS
SM
MD
LG