Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:08

Trump azidi kuongoza miongoni mwa wagombea wa Republican


Bilionea Donald Trump, mgombea urais Marekani anayeongoza dhidi ya wenzie wa Republican
Bilionea Donald Trump, mgombea urais Marekani anayeongoza dhidi ya wenzie wa Republican

Bilionea Donald Trump anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kugombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican mwaka 2016 ambapo Jumapili aliwashambulia wakuu wa makampuni wanaojipatia mishahara mikubwa akisema ni jambo lisilokubalika.

Trump alikiambia kipindi cha “Face the Nation” katika televisheni ya CBS ya nchini Marekani kwamba “unaona watu hawa wanalipwa fedha nyingi na kwa jumla ni kama mzaha”. Katika kampeni za kisiasa nchini Marekani, wagombea wa Democratic mara kwa mara wanakosoa ukosefu wa uwiano kati ya malipo ya wakuu wa makampuni makubwa na wafanyakazi wao, tofauti ambayo inaweza kuwa kubwa kwa mara 350.

Donald Trump akizungumza mjini Washington DC.
Donald Trump akizungumza mjini Washington DC.

Lakini wa-Republican mara kwa mara wanafikiriwa kuwa sehemu ya biashara kubwa nchini Marekani na ni nadra sana kushambulia mishahara ya wakuu wa makampuni na wale wa Wall Street.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 69 mara kwa mara anatamba kuhusu utajiri wake na mafanikio ya biashara katika kujenga majengo marefu huko New York. Lakini alielekeza lawama kwa malipo makubwa wanayolipwa wakuu wa makampuni ambao alisema huwaweka marafiki zao kwenye bodi za wakurugenzi wa kampuni ambao wanaidhinisha mishahara mikubwa kwa viongozi wa kampuni.

XS
SM
MD
LG