Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 21:04

Sasa Trump asema anaamini kuwa Obama alizaliwa Marekani


Campaign 2016 Trump
Campaign 2016 Trump

Kampeni ya mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump, alikubali siku ya Alhamisi kuwa Rais barack Obama alizaliwa Marekani, baada ya miaka kadhaa ya kuhoji juu ya uraia wa rais Obama.

Kupitia taarifa, Kampeni hiyo ilisema kuwaTrump alimlazimisha Obama kuonyesha cheti chake cha kuzaliwa na kufunga suala la mahala alipozaliwa rais huyo wakati akiwa madarakani.

Alhamisi asubuhi, Hillary Clinton, katika kampeni yake ya kwanza baada ya kuugua homa ya mapafu ambayo ilimlazimisha kuchukua mapumziko mafupi ya kiafya, aliwaita wafuasi wa Trump kwamba ni “birther movement”. Hillary alinukuu gazeti la Washington Post lililochapishwa Alhamisi ambapo Trump alikataa kusema kama anaamini Obama alizaliwa nchini Marekani na akasema kuwa angejibu swali hilo wakati mwafaka ukifika. Clinton aliwasihi wapiga kura kufanya uamuzi yakinifu kumsitisha Trump na kusema kuwa mfanyabiashara huyo tajiri hastahili kuwa rais ifikapo kwenye Novemba nane.

XS
SM
MD
LG