Hatua hiyo ni ili kushinikiza kuachiliwa kwa mateka waliobaki, akisisitiza onyo lake la awali kwamba watalipia gharama kubwa huko Gaza, iwapo hawatawaachilia mara moja. “Mtajua ninachosema,” Trump alisema akiwa kwenye chumba cha Oval, huko White House, baada ya kuulizwa na mwanahabari alichomaanisha.
Trump pia aliangazia mkutano wake wa Jumatano na baadhi ya mateka waliyoachiliwa. Mapema Alhamisi, mjumbe maalum wa Trump kwa Mashariki ya Kati Steve Witkoff aliwaambia wanahabari huko White House kwamba huenda hatua fulani zikachukuliwa na utawala wa Marekani kwa ushirikiano na Israel. Trump wala White House hawajasema iwapo hatua inayokusudiwa kuchukuliwa dhidi ya Hamas itakuwa ya kijeshi.
Forum