Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 21:38

Trump adai jaji anayesimamia kesi yake anapaswa kubadilishwa


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ahudhuria Kongamano la Kihafidhina la Kisiasa (CPAC) katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Gaylord huko National Harbor, Maryland, Marekani, Machi 4, 2023. REUTERS
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ahudhuria Kongamano la Kihafidhina la Kisiasa (CPAC) katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Gaylord huko National Harbor, Maryland, Marekani, Machi 4, 2023. REUTERS

Trump pia ameongeza kwamba  kesi hiyo ni vyema ihamishwe kutoka Washington Dc ambako wakazi kwa idadi kubwa hawakumpigia kura

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alidai Jumapili kwamba jaji wa serikali kuu alichaguliwa bila mpangilio kusimamia kesi hiyo akimtuhumu kwa njama ya kutaka kubadili kushindwa kwake katika uchaguzi wa mwaka 2020 haitakuwa haki kwake na anapaswa kubadilishwa.

Pia ameongeza kwamba kesi hiyo ni vyema ihamishwe kutoka Washington ambako wakazi kwa idadi kubwa hawakumpigia kura na jopo la mahakama linatarajiwa kuchaguliwa kutoka kwenye kundi la wapiga kura waliojiandikisha wa mjini humo.

Trump katika mtandao wake wa Truth Social aliandika kwa herufi kubwa ‘kwamba hakuna njia naweza kuwa na kesi ya haki na hakimu aliyepewa aendeshe kesi akimzungumzia Jaji wa Mahakama ya Wilaya Tanya Chutkan.

Mahakama ya Wilaya ya Washington DC hakujibu mara moja ombi la Reuters kutoa maoni yake.

Forum

XS
SM
MD
LG