Trump alizungumza na maafisa wa ngazi ya juu wa kampuni ya magari ya Ford, General Motors na Stellantis kabla ya kutangaza kuchelewesha, msemaji wa White House, Karoline Leavitt aliwaambia wanahabari.Alisema kwamba Trump aliwasihi watengeneza magari hao kuhamisha viwanda vyao kutoka Mexico na Canada hadi Marekani, ili kuepuka kulipa ushuru.
Hata hivyo ushuru mpya kwenye bidhaa nyingine kutoka Mexico na Canada bado upo, ingawa Leavitt alisema kuwa rais yuko tayari kwa mazungumzo ya kutafuta mbadala.Trump alitangaza uchelewesho wa ushuru wa magari baada ya kuongea awali na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ambapo kwa kwa mujibu wa Associated Press, Canada haipo tayari kuondoa ushuru iliyouweka kama Trump ataacha ushuru mwingine kwa Canada.
Forum