Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:32

Trump anaanza ziara yake ya kimataifa kama Rais


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump anaanza ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama rais Ijumaa, huku akiiwacha ikulu imegubikwa na utata mkubwa kuhusu uhusiano kati ya timu yake ya kampeni na Russia na shutuma za kuingilia kati uchunguzi wa Michael Flynn.

Utata huo unaouhusisha utawala wa Trump na udukuzi wa Russia umepelekea baadhi ya wanasiasa kuufananisha na kashfa ya Watergate, iliyouangusha utawala wa rais Richard Nixon mnamo mwaka wa 1973.

Hata hivyo, rais Trump aliwaambia waandishi wa habari jana Alhamisi kwamba anatumai mizozo iliyokuwa imeukumba utawala wake itatatuliwa siku za karibuni.

Mgogoro huo ni pamoja na kufutwa kazi kwa aliyekuwa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ( FBI), James Comey, huku kukiwa na tuhuma kwamba Trump alimtaka Comey kusitisha uchunguzi dhidi ya aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa, Michael Flynn.

Rais Trump pia anakabiliwa na maswali kuhusu uhusiano wake na Russia wakati wa kampeni za urais za mwaka jana, na kwamba huenda alitoa habari za siri za kijasusi, kwa waziri wa mambo ya nje wa Russia, wakati wa mkutano uliofanyika kwenye afisi ya rais katika ikulu ya White House.

Ziara ya Trump itampeleka hadi Saudi Arabia, Vatican na Israeli maeneo yaliyo matakatifu kwa dini tatu kuu ulimwenguni, Uislam, Ukristo na Uyahudi.

Akiwa Saudi Arabia, Trump ambaye amekuwa akisema kuwa hawaamini Waislam na amejaribu kupiga marufuku Waislam kuingia Marekani, anatarajiwa kutoa hotuba kuhusu Uislam mbele ya kikundi cha viongozi wa Kiislamu.

H. R McMaster, ambaye ni mshauri wa usalama wa taifa wa Trump amesema rais anamatarajio makubwa kwa kupatikana mwelekeo wa amani wa Uislam.

Pia kuna utata ulioifungamana na ziara ya rais wa Marekani atakayoifanya Israeli, kufuatia madai kwamba alitoa siri za kiusalama za Israeli kwa maafisa wa Russia.

XS
SM
MD
LG