Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 17:54

Trump aahidi kuliunganisha taifa


Rais mteule Donald Trump na mkewe Melania Trump
Rais mteule Donald Trump na mkewe Melania Trump

Rais mteule, Donald Trump ameahidi kufanya kazi kwa bidii, kuliunganisha taifa na “kuifanya Marekani kuwa bora kwa kila mtu.”

Katika kilele cha siku ya kuapishwa kwake, Trump ametabiri kuwa taifa “litashuhudia maajabu “ siku ya Ijumaa wakati akiapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.

Baada ya maonyesho yakiwa ni sehemu ya sherehe za kuapishwa kwake Alhamisi usiku katika ngazi za jengo la kumbukumbu ya Lincoln; mmoja wa waasisi wa taifa hili, Trump amesema wazi kwamba hajali iwapo hali ya hewa itakuwa shwari au kutakuwa na mvua,” akiwaambia maelfu waliohudhuria kuwa ulimwengu unashuhudia kile kinachotokea Marekani.

Mambo yatabadilika

Sean Spicer, ambaye atakuwa msemaji wa Trump katika ikulu ya White House, amesema rais mteule amekuwa akiendelea kufanya mabadiliko katika hotuba yake ya kuapishwa ambayo ataitoa katika ngazi za jengo la bunge la Marekani mchana wa siku ya Ijumaa.

Spicer amesema hotuba yake itakuwa “ yake mwenyewe na ni dira yake kwa ajili ya Marekani.”

Trump anakusudia kuainisha “ changamoto zinazotukabili” katika hotuba yake, Spicer aliongeza. Ameelezea kuwa ujumbe wake wenye kauli ya kifalsafa inayoonyesha wapi Trump anataka kuipeleka serikali ya kitaifa, lakini sio ajenda ya kisheria.

Kuanzia Ijumaa mchana na pia kwa siku kadhaa baada ya hapo, msemaji huyo amesema Trump ataweka saini amri za kirais “ zitakazoweka ajenda ya mabadiliko ya kweli.” Rais mteule bado “ anafanyia kazi maeneo ambayo anataka kuchukua hatua na kwa mpangilio gani,” Spicer ameongeza.

Trump anaweza kubadilisha mara moja baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na Rais Barack Obama kwa hatua hizo.

Niko tayari kulitumikia taifa

Makamu rais mteule, Mike Pence amesema yeye na Trump watakuwa “tayari kuwatumikia watu wa Marekani siku ya kwanza watakapochukua madaraka.”

Kuhusu kuteuliwa kwa aliyekuwa Gavana wa Georgia Sonny Perdue kuwa waziri wa kilimo, Spicer amesema, Trump ameshajaza nafasi zote 21 za baraza lake la mawaziri.

Pia ameeleza kuwa maafisa 536 tayari wameshawekwa katika idara mbalimbali katika jiji la Washington ilikuungana na mabadiliko ya uongozi wakati serikali itakapoanza kazi rasmi Jumatatu.

Spicer amesema maafisa 50 waliokuwa wakishughulikia shughuli za serikali ya Marekani katika uongozi wa Obama wamekubali kuendelea kuwepo katika utawala mpya.

Makamu rais mteule amesema Trump ameshaweka mipango ya “siku ya kwanza ofisini, siku ya 100, na siku ya 200” juu ya aina za sera uongozi huu mpya unatarajia kutekeleza. Utashi wa watu kufanya kazi na utawala huu mpya umeongezeka kila siku, Pence ameongeza kusema, ikiwa tayari watu 86000 wameshaomba nafasi za kazi.

Trump na Pence, washindi wa moja ya chaguzi ya Kitaifa ya Marekani iliyokuwa na utata mkubwa, walihudhuria matukio kadhaa katika jiji la Washington Alhamisi.

Trump amewapongeza wateule wake wakati wa hafla ya chakula cha mchana katika hoteli ya Trump International, iliyoko karibu na ikulu ya White House. Alitangaza wakati huo kuwa alikuwa na nia ya kumteua Woody Johnson, bilionea anayemiliki timu ya mpira wa kulipwa ya New York Jets, kuwa balozi wa Marekani nchini Uiingereza.

Rais mteule Donald Trump na Makamu wake Mike Pence
Rais mteule Donald Trump na Makamu wake Mike Pence

​Baadaye, akiwa amefuatana na Pence, Trump aliweka shada la maua huko kwenye makaburi ya mashujaa wa kitaifa Arlington, Virginia ambako zaidi ya mashujaa wa kivita 400,000 na familia zao wamezikwa.

Jioni, Trump na Pence, pamoja na maafisa wa juu katika uongozi mpya, walitarajiwa katika chakula cha usiku maarufu kama Candlelight (taa ya mshumaa) wakijumuika na wafadhili wa kampeni kwenye kituo kikubwa cha treni kinachojulikana kama Union Station huko Washington.

Apumzika Blair House

Trump amekuwa akipumzika katika usiku wa mwisho kama raia wa kawaida katika nyumba ya Blair, ambayo ni nyumba ya serikali kwa ajili ya makazi ya viongozi, iliyoko upande wa mtaa wa Pennsylvania ukitokea ikulu-White House.

Hata baada ya matayarisho ya kuapishwa rais—pamoja na shamra shamra na maandalizi rasmi yanayofanyika kwa ajili ya kukabidhiana madaraka Marekani wakati ambao Obama anaachia madaraka baada ya miaka minane kama kiongozi wa Taifa la Marekani—wateule wawili wa baraza la mawaziri la Trump bado wanakabiliwa na mahojiano ya kuthibitishwa kwao mbele ya kamati za Seneti.

Gavana wa zamani wa Texas, Rick Perry, ambaye ameteuliwa na Trump kama waziri wa nishati, amesema anajuta kwa kauli aliyoitoa—wakati wa kinyang’anyiro cha kugombea urais 2012- pale aliposema kuwa anataka wizara ya nishati ifutwe ambayo hivi sasa anatakiwa kuiongoza.

Mteule wa wizara ya fedha, Steve Mnuchin amekabiliwa na masuali magumu kuhusu usimamizi wake wa benki ambazo zilisababisha matatizo kuwepo mikopo isiyoweza kulipika, iliyopelekea watu kupoteza nyumba zao wakati wa matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba Marekani mwaka 2009.

Lakini msemaji Spicer amemkosoa Seneta Chuck Schumer, kiongozi wa wlio wachache wa chama cha Demokratik kwenye seneti, kwa kuchelewesha mipango ya wa Republikan kuwathibitisha wateule wao waliochaguliwa na Trump katika baraza la mawaziri mara moja.

Hata wale “wanaokubalika pande zote” kwa nafasi za mawaziri bado wanangoja kuthibitishwa, Spicer amesema. “Hakuna udhuru wowote kwa mbinu za ucheleweshaji kama huu.”

Baadhi ya mawaziri wateule wamekuwa wakikabiliwa na hali ngumu kuthibitishwa katika mahojiano, ikiwa wa Demokratiki wakiendelea kuibua masuali mengi kuhusu masuala binafsi ya miradi ya kifedha, utata juu ya mahusiano yao na wizara hizo walioteuliwa kuziongoza na pia kutokuwa na maarifa juu sharia na sera zilizopo katika wizara hizo.

XS
SM
MD
LG