Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 21:52

Trump aahidi kukabidhi biashara kwa watoto wake wa kiume


rais mteule wa Marekani, Donald Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump alisema atazungumza na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusu uteuzi wake wa baraza la mawaziri pamoja na biashara yake ambayo atawakabidhi watoto wake wa kiume.

Tangazo hilo lilitolewa Jumatatu jioni kwenye mtandao wa Twitter limekuja siku kadhaa kabla ya hivi sasa jinsi atakavyojitenga na biashara zake kwa maslahi ya ulimwengu ili kulenga katika urais na kuepuka mizozo ya kimaslahi binafsi.

Mshauri wake mmoja alisema Jumatatu kwamba taarifa za kina kuhusiana na hilo zitatolewa wakati wowote mwezi Januari. Trump aliandika kwamba kabla ya Januari 20 siku ambayo ataapishwa rasmi kuwa rais wa Marekani ataacha biashara zake chini ya utawala wa watoto wake wa kiume, Don na Eric, pamoja na wakurugenzi wengine. Aliahidi zaidi kwamba hakuna makubaliano mapya yatakayofanywa wakati wa muda wake akiwa madarakani.

XS
SM
MD
LG