Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:25

Timu za Afrika Mashariki zakosa fainali za Afrika


Fainali za kombe la mataifa Afrika 2012 kufanyika E. Guinea na Gabon
Fainali za kombe la mataifa Afrika 2012 kufanyika E. Guinea na Gabon

Misri, Nigeria, Cameroon, Algeria na Afrika Kusini miongoni mwa miamba itakayokosa fainali za mwaka 2012

Timu za kandanda za Afrika Mashariki na eneo la maziwa makuu zote zimeshindwa kuingia fainali za kombe la Afrika mwakani zitakazochezwa Equatorial Guinea na Gabon kuanzia Januari 21 mwakani.

Uganda ambayo ilikuwa na nafasi nzuri baada ya kuongoza kundi lake kwa muda mrefu ilishindwa kuingia fainali baada ya kuwekewa ngumu na ndugu zao wa Kenya na kutoka sare ya 0-0 Jumamosi. Tanzania nayo ilichapwa 3-1 na Morocco hivyo kumaliza kabisa uwezekano wake wa kuingia fainali hizo.

DRC ilifungwa 3-2 na Cameroon Ijumaa ingawa matokeo hayo hayakuisaidia Cameroon kuingia fainali. Rwanda ilimaliza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Benin wakati Burundi ilifungwa 2-1 na Ivory Coast

Kwa ushindi wake dhidi ya Tanzania, Morocco ilifanikiwa kuungana na Sudan kuchukua nafasi mbili za mwisho katika fainali hizo za mwaka 2012 baada ya Jamhuri ya Afrika Kati (CAR) kufungwa 2-0 na Algeria. Kufungwa kwa CAR ndio kulikoisaidia Sudan kuingia fainali baada ya kuchukua nafasi ya pili katika kundi I lililoongozwa na Ghana.

Niger na Botswana zimeandika historia kwa kuingia katika fainali zao za kwanza. Timu ambazo zimefanikiwa kuingia fainali ni wenyeji Equatorial Guinea na Gabon, washindi wa makundi Mali, Guinea, Zambia, Morocco, Senegal, Burkina Faso, Niger, Ivory Coast, Ghana, Angola na Botswana. Libya na Sudan zimeingia kama washindi wa pili wa juu kutoka makundi yote.

XS
SM
MD
LG