Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 21:32

Timu ya US Monastir ya Tunisia yaanza na ushindi michuano ya BAL


Aten James Majok double-double sparks US Monastir over Beira in Dakar Arena on Sunday.(Photo BAL).

Timu ya US Monastir mabingwa wa Tunisia walitoka kifua mbele katika mechi yao dhidi ya Ferroviário da Beira ya Msumbiji kwa jumla ya pointi 77-71 katika uwanja wa Dakar Arena Senegal jumapili.

Timu ya US Monastir mabingwa wa Tunisia walitoka kifua mbele katika mechi yao dhidi ya Ferroviário da Beira ya Msumbiji kwa jumla ya pointi 77-71 katika uwanja wa Dakar Arena Senegal jumapili.

Alikuwa ni mchezaji hatari wa Monastir Aten James Majok aliyewachachafya mabingwa wa Msumbiji CFV Beira kwa kupachika jumla ya pointi 19 huku wachezaji Kennedy na William perry wakifunga pointi 17 kila mmoja kwa timu ya CFV Beira licha ya kupoteza mchezo huo.

Majok mzaliwa wa Sudan mwenye asili ya Australia na Lebanon alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kwa kuongoza kwa jumla ya pointi 19, rebaundi 12 na mipira ya kuzuia 4.

Naye mchezaji wa kimataifa wa Tunisia Firas Lahyani alimaliza akiwa na pointi 15 na mwenzake Michael Dixon alimaliza akiwa na pointi 14 kwa washindi hao wa pili wa msimu wa uzinduzi wa BAL US Monastir ya Tunisia.

Joyce Muchenu kutoka Zimbabwe aliweka rekodi nyingine ya kuwa refa mwanamke katika michuano ya BAL kwenye mchezo huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG