Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 12:31

Timu ya REG ya Rwanda yaangusha vigogo wa Morocco AS Sale


Mamadi Keita (S.L.A.C.), BAL President Amadou Gallo Fall and Abel Abdourahmane Diop (DUC) at BAL 2022 opening game in Dakar, Senegal.
Mamadi Keita (S.L.A.C.), BAL President Amadou Gallo Fall and Abel Abdourahmane Diop (DUC) at BAL 2022 opening game in Dakar, Senegal.

Ilikuwa ni mechi yenye ushindani mkali ambapo hatimaye Mabingwa wa Rwanda (REG) waliibuka kidedea kwa kuwashinda AS Sale ya Morocco 91 kwa 87 katika  mchezo wa pili wa msimu wa pili wa Ligi ya Mpira wa Kikapu barani Afrika BAL.

Mchezaji wa Rwanda Dieudonne Ndayisaba Ndizeye alitumbukiza mpira kwenye kikapu katikati ya robo ya kwanza ili kutokuwa nyuma sana ya timu ya Morocco.

REG walikuwa nyuma kwa muda mwingi wa mchezo wa kwanza wa Jumapili wa Kongamano la Sahara dhidi ya Association Sportive de Salé ya Morocco, lakini mara walipogeuza mchezo, hawakurudi nyuma.

Jean Jacques Nshobozwabyos enumukiza alitoka kwenye benchi kucheza nafasi ya kishujaa baada ya kujitolea katika maeneo yote uwanjani.

Mchezaji huyo mwenye nafasi ya ulinzi huyo mwenye umri wa miaka 23 alimbana vilivyo mfungaji bora wa AS Salé Terrell kwa zaidi ya robo ya tatu, lakini pia alimaliza na kuwazima mabingwa hao wa Morocco katika mchezo huo kwa pointi tatu ikiwa imesalia dakika moja na kusaidia timu yake iliyofuzu kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya BAL REG kuwaangusha mabingwa wa zamani wa Afrika.

Wakiwa mbele kwa pointi mbili katika robo ya nne, Filer alitoa pasi kwa Anthony Rashad Walker ambaye alifunga kwa mkono mmoja.

Filer aliendelea na pasi kwa Elie Kaje ambaye alikosa nafasi ya kufunga pointi tatu lakini Cleveland Joseph Thomas alikuwepo kufunga kwa mpira wa rebaundi na kuongeza pointi kwa timu yake.

Huku zikiwa zimesalia dakika 7 mchezo kumalizika, Filer alimpatia tena pasi Walker akaweka ndani na kuongeza uongozi wa REG.

Wakiwa chini kwa pointi 3 zikiwa zimesalia dakika 4, Khalid Boukichou wa AS Sale anapoteza udhibiti wa mpira, huku Walker wa Rwanda akimpatia pasi Cleveland Joseph Thomas Jr. na kupachika pointi mbili.

Terrel De Von Stoglin wa AS Sale alipachika pointi mbili ikiwa imesalia dakika moja na nusu na wakiwa chini kwa pointi 3, lakini vijana wa REG kutoka Rwanda waliibuka na ushindi.

XS
SM
MD
LG