Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:21

Timu ya Comoro yakumbwa na pigo la Covid nchini Cameroon


Wachezaji wa timu ya taifa ya Comoro wakishangilia baada ya kuifunga Ghana mabao 3-2 na kuiondoa kwenye michuano hiyo mapema.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Comoro wakishangilia baada ya kuifunga Ghana mabao 3-2 na kuiondoa kwenye michuano hiyo mapema.

Timu ya Comoro iliyoweka historia kwenye michuano ya fainali ya Kombe la Afrika,wiki hii, kwa kuingia raundi ya pili baada ya kuilaza Ghana mabao 3-2 imekumbwa na tatizo kubwa baada ya wachezaji na maafisa12 katika timu yao kupimwa na na kupatikana na virusi vya corona. 

Akizungumza na Sauti ya Amerika msemaji wa timu hiyo Bi.Mirna Bourhane anasema kwamba walinda mlango wawili wa ziada ni miongoni mwa waliopimwa na kupatikana virusi vya Corona. Anasema golikipa wao Salim Ben Boina yungali mgonjwa baada ya kujeruhiwa bega wakati wa mechi yao na Ghana.

Habari hizi zimetolewa siku mbili tu kabla ya mchuano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na muhimu dhidi ya Cameroon siku ya Jumatatu wanapoanza michuano wa raundi ya 16.

Bourhane anasema wamewasilisha malalamiko mbele ya Shirikisho la Kandana la Afrika na FIFA, kudai kufanyiwa vipimo vipya na wameahidiwa itafanyika siku ya Jumapili.

Kocha wa time ya Ceolacanth, Amir Abdou anaesifiwa kwa kuiongoza timu hiyo kwa miaka minane sasa na kuifikisha mahala ilipo hii leo pia amelazimika kujiweka katika karantini.

Msemaji wa timu Bourhane anasema kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa wachezaji kwani yeye ndiye kiungo muhimu wa timu hiyo.

Kwa ujumla ni wachezaji saba walopimwa na virusi vya Corona na kulingana na kanuni za CAF ni kwamba mechi itakayoahirishwa ikiwa timu inawachezaji 11 waliyo katika afya nzuri, Na hata ikiwa hawana golikipa mchezaji mmoja wa mbele anaweza kuchukua nafasi hiyo.

Kufuatana na habari VOA imepata ni kwamba tayari kuna golkeepa Bravador kutoka Ufaransa yuko njiani kuelekea Yaunde ambako Comoro itapambana na wenyeji wa michuano Simba wa Cameroon.

Wakomoro kote nchini wamesikitishwa sana na wanafanya dua na sala katika kuiombea timu yao kuweza kushiriki na kufanikiwa.

XS
SM
MD
LG