Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 05:05

Michuano ya raundi ya 16 ya AFCON kuanza Jumapili.


Wachezaji wa Cameroon wakishangilia ushindi dhidi ya Ethiopia na sasa wanafungua raundi ya 16 na Comorro.CAN 2021

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika siku ya Jumapili inaingia katika  awamu ya 16 ya michuano hiyo  ya TotalEnergies inayoendelea, Cameroon 2021 na pazia litafunguliwa na timu za Burkina Faso na Gabon zikimenyana huko Limbe.

Vile vile siku hiyo Timu ya Nigeria-Super Eagles itamenyana na Carthage Eagles ya Tunisia huko Stade Roumde Adjia, mjini Garoua.

Timu ya Gabon inaingia hatua hiyo ikiwa inawakosa nyota wake watatu Pierre Aubomayeng, Axel Meye na Mario Lemina kutokana na matatizo ya moyo baada ya kupatwa na covid-19. Lakini timu hiyo imeonyesha moyo mkubwa wa kupambana na kuingia hatua hiyo bila wachezaji hao muhimu na kutangaza kwamba hiyo inawasukuma kupambana kila wakati.

Hii itakuwa mechi ya tatu ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Burkina Faso na Gabon, huku Gabon ikiwa haijashindwa katika mechi mbili zilizopita zote katika hatua ya makundi (2-0 mwaka 2015 na 1-1 mwaka 2017).

Burkina Faso wamepoteza mechi moja pekee kati ya tisa zilizopita za Kombe la Mataifa ya Afrika wakishinda michezo mingi katika matoleo yao mawili ya mwisho ya AFCON kama walivyopoteza katika ushiriki wao mara 10 zilizopita.

Gabon hawajashindwa katika mechi zao sita zilizopita za Kombe la Mataifa ya Afrika, ingawa wameshinda mechi moja tu kati ya nane zilizopita kwenye shindano hilo tangu ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso mwaka 2015.

Na katika mpambano mwingine siku hiyo kati ya Nigeria na Tunisia kutakuwa na kazi kubwa huku timu ya Nigeria ikiingia nafasi hiyo baada ya kufanya vyema katika hatua ya makundi ikishinda mechi zake zote.

Huku Tunisia ikiwa imeingia kama moja ya timu bora katika nafasi ya tatu baada ya kupoteza mechi mbili na kushinda moja tu katika kundi lake.

Tunisia ipo katika hali ngumu baada ya baada ya wachezaji wengine saba kukutwa na virusi vya Corona kabla ya mechi yao ya mwisho ya Kundi F dhidi ya Gambia siku ya Alhamisi ikiwa ni pamoja na nahodha wao nyota Wahbi Al-Kazri.

Nigeria inaongozwa na nahodha wake William Ekong kadhalika ikiwa na wachezaji wengine hatari kama vile Kelechi Iheanacho, Wilfred Ndidi, Mosses Simon na wengineo.

Nigeria ilifuzu kwa pointi tisa, ikiwa ni idadi ya juu zaidi katika hatua ya makundi.

Wachambuzi wanatarajia kuona maajabu kuonekana katika hatua hii ya makundi ikiwa imeshuhudiwa timu nyingi zimeingia zisizo na majina kama vile Comoro ambao wameingia kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo, Malawi ambao wanaingia kwa mara ya hatua hii ya 16 bora na CapeVerde taifa dogo lililoshangaza dunia mwaka 2013 lilipoingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG