Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:13

Gavana wa Lamu atoka jela kwa dhamana


Gavana wa Lamu Issa Timamy
Gavana wa Lamu Issa Timamy

Mahakama moja ya Mombasa imemtoa gerezani Gavana wa Lamu Issa Timamy kwa dhamana ya shillingi millioni 20 za Kenya baada ya kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya jumla, ugaidi na kuondoa watu makwao.

Bwana Timamy alikamatwa wiki iliyopita kuhusiana na mauaji ya watu wapatao 65 yaliyotokea Lamu katika kijiji cha Mpeketoni. Gavana huyo amedia kuwa kukamatwa kwake ni njama za makundi ya rushwa na vyombo vya serikali vinavyomtaka aondoke madarakani kufungua njia ya kufuja mali ya umma.

Timamy ambaye alikutana na kamati yake ya utendaji kutoka county yake akiwa mikononi mwa polisi Jumamosi katika juhudi za kuendeleza utawala wake, anadai kuwa kukamatwa kwake ni kazi ya Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph ole Lenku, Inspekta Mkuu wa polisi David Kimaiyo na Kamishna wa Country ya Lamu Stephen Ikua.

XS
SM
MD
LG