Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:58

Tillerson aahidi kupunguza matumizi wizara ya mambo ya nje


Rex Tillerson, mwenyekiti wa zamani wa Exxon Mobil akitoa ushuhuda huko Capitol Hill. Jan 11, 2017.
Rex Tillerson, mwenyekiti wa zamani wa Exxon Mobil akitoa ushuhuda huko Capitol Hill. Jan 11, 2017.

Tillerson atakuwa makini juu ya China, hususan katika suala la harakati zake za kijeshi katika maji yenye mgogoro katika bahari ya South China.

Waziri mteule wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani aliyeteuliwa na rais mteule, Donald Trump Jumatano aliahidi kurekebisha wizara hiyo kuifanya iwe bora zaidi na kupunguza matumizi.

Tillerson, aliwaambia maseneta wakati wakisikiliza ushuhuda wake kuwa atakuwa makini juu ya China, hususan katika suala la harakati zake za kijeshi katika maji yanayozozaniwa katika bahari ya South China.

Mojawapo ya masuala yaliyozusha wasi wasi kwa maseneta ilikuwa iwapo kazi aliyofanya kwenye moja ya kampuni za mafuta itabadilisha mtazamo wake wa ulimwengu.

Lakini maswali mengi kutoka kwa maseneta yalihusu uhusiano wa Tillerson na Russia. Wakati alipokuwa mkuu wa kampuni ya Exxon, Tillerson aliingia mikataba na makampuni ya mafuta ya Russia. Maseneta walitaka kufahamu vipi atashughulikia suala la udukuzi waliofanyiwa wanasiasa wa Marekani na kuwanyanyasa washirika wa Marekani.

Tillerson amesema, "wakati ushirikiano na Russia unahusu maslahi sawa, kama vile kupunguza vitisho vya ugaidi, pia ni vyema tuangalie njia mbadala. Pale ambako kuna tofauti muhimu, lazima tuwe haraka katika kutetea maslahi ya Marekani na washirika wake. Russia ni vyema ifahamu kwamba tutawajibika kwa vitendo vyetu na vile vya washirika wetu, na kwamba Russia ni vyema nayo iwajibike kwa vitendo vyake."

XS
SM
MD
LG