Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:06

Mikataba ya ulinzi kuiimarisha Saudi Arabia dhidi ya vitisho vya Iran


Ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Rais Donald Trump kabla ya kuanza kwa mkutano wa pamoja na viongozi wa Saudi Arabia
Ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Rais Donald Trump kabla ya kuanza kwa mkutano wa pamoja na viongozi wa Saudi Arabia

Makubaliano ya ununuzi wa silaha za thamani ya dola za Kimarekani bilioni 110 ambayo yamesainiwa na Marekani na Saudi Arabia Jumamosi yanakusudia kutokomeza uchochezi hatarishi wa Iran.

Hayo yamesemwa Jumamosi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson wakati wa mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja Riyadh na Waziri wa Mambo ya Nje Adel al-Jubeir, Tillerson amesema mkataba huo wa ulinzi umekusudia kusaidia “mkakati wa ulinzi wa muda mrefu wa Saudi Arabia na eneo lote la Ghuba ya Uajemi.”

Mkataba huo tayari umekwisha pitishwa, Tillerson amesema, “katika hali ya hivi sasa ya kupambana na kampeni hatarishi ya Iran na vitisho vyake, ambavyo vipo katika maeneo yote ya mipaka ya Saudi Arabia.”

Mkataba huo wa ulinzi ambao unaanza mara moja, ni moja kati ya mtiririko wa mikataba iliyosainiwa Jumamosi na Mfalme wa Saudi Arabia Salman na Rais Donald Trump.

Imelenga katika kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili na unajumuisha mkataba wa pili wa ulinzi ambao unahiari mbalimbali zenye thamani ya mpaka dola billioni 350 kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

Tillerson amesema lengo la Trump kufanya ziara Saudi Arabia ilikuwa kukabiliana na aina yoyote ya vitisho vinavyofanywa na Iran. Amesema mlolongo wa mikutano ya hadhara na ya ndani ambayo Trump amekuwa akiifanya inalengo la “kupeleka ujumbe mzito kwa maadui zetu wanaofanana.”

Tillerson amemtaka rais aliyechaguliwa tena Iran Hassan Rouhani kutumia kipindi chake cha pili madarakani kusitisha programu ya kombora la balistiki nchini humo na tabia ya nchi yake kusaidia magaidi.

XS
SM
MD
LG