Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 11:55

Tillerson aahidi kuendeleza uhusiano wa Marekani - Afrika


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Afrika Moussa Faki
Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Afrika Moussa Faki

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson ameahidi kwa mara nyingine mshikamano wa Marekani na nchi za Afrika, katika juhudi za kufuta kauli ya utata iliotolewa na Rais Donald Trump ikilikashifu bara hilo.

Mkutano wa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani alioufanya na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki umekuja miezi miwili baada ya kuripotiwa kuwa Trump alitumia maneno machafu kuelezea nchi ya Haiti na baadhi ya nchi za Afrika.

Umoja wa Afrika na serikali kadhaa za Afrika walikuwa wamekasirishwa na matamko hayo ya Trump.

“Nafikiri ahadi ya mafungamano ya Marekani na nchi za Afrika iko wazi juu ya umuhimu tunaotoa katika ushirikiano huu. Rais ameandika barua yake binafsi kwenda AU,” amesema Tillerson katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Faki huko makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Faki amesema alipokea barua iliyoandikwa Januari 25 na “tukio hili” tayari ni “jambo lililopita.”

Faki ameongeza kuwa ziara ya mwanadiplomasia wa juu wa Marekani ni ushahidi kuwa mahusiano kati ya Afrika na Marekani bado ni imara.”

Tillerson amesema kuwa kuhamasisha amani na usalama, maendeleo na biashara, na utawala bora ni nguzo tatu zinazotumiwa na Washington katika kushirikiana na Afrika.

XS
SM
MD
LG