.Hatua hiyo inadaiwa ni kutokana na kuunga mkono waandamanaji wanaopinga utawala wa kifalme wenye nguvu nyingi nchini humo. Seksakol Atthawong ambaye ni naibu waziri kwenye ofisi ya waziri mkuu ameiambia voa mwishoni mwa wiki kwamba tayari ana sahihi milioni moja, zilizoanza kukusanywa mwaka jana, na kwamba ataziwasilisha kwenye wizara ya mambo ya ndani na usalama wa kitaifa hapo Alhamisi.
Kupitia mtafsiri wake, Attawong amesema kwamba Amnesty inashirikiana na watu wanaopinga katiba ya Thailand iliyoko chini ya utawala wa kifalme. Kundi wa waandamanaji likiongozwa na vijana lilianza mwaka wa 2019, wakati likiitisha kujiuzulu kwa Prayut, lakini baadaye likaongeza masuala mengine 10 yanayohitajika kubadilishwa kwenye katiba ili kudhibiti uwezo wa kisiasa wa utala huo wa kifalme.