Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 06:45

Thailand inataka kuingia BRICS


Thailand inataka kuwa mwanachama wa kwanza wa BRICS kutoka Kusini Mashariki mwa Asia, kundi la mataifa ya kikanda kwa nchi zinazoendelea zikiwemo Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.

Baraza la Mawaziri la Thailand liliidhinisha rasimu ya barua ya maombi Mei 28, ikionyesha nia ya nchi hiyo kujiunga na kundi hilo.

Wataalam wanaona uanachama huo wa Thailand, ambayo ina uchumi mkubwa wa pili katika Asia Kusini, utakuwa kama wa nembo kuliko kuwa na mafufaa zaidi ikijumuisha makubaliano ya biashara huria na nchi kama vile China.

Hata hivyo, utawala wa Waziri Mkuu, Srettha Thavisin, unapanga kuendelea na ombi hilo wakati wa mkutano wa mwaka wa BRICS, utakaofanyika Oktoba, mjini Kazan, Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG