Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:42

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 5.0 latikisa majengo karibu na Johannesburg


Ramani ya Afrika Kusini

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 5.0 Jumapili limetokea karibu na Johannesburg, na kutikisa majengo katika mkoa wenye watu wengi nchini Afrika Kusini, taasisi ya Marekani ya masuala ya jiolojia imeripoti.

Majengo yalitikiswa katika mkoa wote wa Gauteng ambako mji mkubwa wa Johannesburg na kitovu cha biashara nchini humo unapatikana.

Wakazi kote katika mkoa huo walihisi tetemeko hilo na wengine walichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha uharibifu mdogo wa kuta za nyumba.

Idara ya huduma za dharura haikuripoti vifo wala majeruhi lakini ilisema wafanyakazi wake wa kudhibiti majanga wataendelea kuwa tayari kukabiliana na athari zinazoweza kutokea.

Msemaji wa idara ya huduma za dharura katika mji wa Johannesburg Xolile Khumalo amewaonya wakazi kuwa macho endapo tetemeko la ardhi litatokea.

Forum

XS
SM
MD
LG