Wataalam wameonya kuwa mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika siku chache zijazo huenda ikavuruga juhudi za uokoaji.
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.3 kwa kipimo cha rikta, lilipiga kisiwa hicho cha kusini magharibi mwa Pacific Jumanne na kuua watu 14.
Zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa.
Tetemeko jingine la ukubwa wa 6.1 kwa kipimo cha rikta lilipiga kwa mara nyingine Jumapili na kuongeza matatizo zaidi.
Mojawapo ya changamoto kubwa kwa sasa ni matetemeko mengine ya ardhi yanayoendelea kutokea.
Port Villa imeshuhudia matukio kadhaa ya matetemeko ya ardhi na kuathiri shughuli za biashara.
Ardhi haina uwezo wa kustahimili uzito na matukio zaidi ya matetemeko ya ardhi.
Maafisa wamesema kwamba juhudi za uokoaji hazitaendelea hadi watakapohakikisha usalama wa waokoaji.
Forum