Wandayi amesema kuwa kukataa kwa IEBC kusitisha tenda pamoja na kuweko kinyongo kwa baadhi ya makundi kunatia wasiwasi.
Seneta James Orengo na Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi wamesema watafanya "kila kile watachoweza" ikiwepo hatua ya kupeleka malalamiko yao katika mahakama ya juu nchini Kenya, wakipinga uamuzi uliofanywa kuwapa tenda kampuni ya Al-Ghurair.
Lakini IEBC imeendelea kunang’ania uamuzi wake pamoja na suala zima kugubikwa na mgogoro huo wa manunuzi, wakati Nasa Jumamosi imetishia kuchukua hatua za kisheria kusimamisha tenda hiyo ya uchapishaji wa karatasi za kupiga kura iliyotolewa kwa kampuni ya Al Ghurair.
Siku ya Jumamosi, Mkurugenzi mtendaji wa IEBC, Ezra Chiloba ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa taasisi hiyo aliyetajwa na Nasa kushutumiwa kufanya upendeleo katika kutoa tenda hiyo kuwapa Al Ghurair.
Pia ameliambia gazeti la Nation kwamba Tume itatembelea Dubai kwenye kampuni hiyo ya uchapishaji kama ilivyopangwa pamoja na kuwa Jubilee na Nasa kueleza kuwa hawatatuma wawakilishi wao katika safari hiyo ilioandaliwa Juni 22.