Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 15:16

Tedros kuwania tena ukuu wa WHO


Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom

Ripoti kutoka vyanzo vya kutegemewa zinasema kuwa mkuu wa shirika la afya duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, anapanga kuwania nafasi hiyo kwa muhula wa pili wa kipindi cha miaka mitano.

Tedros mwenye asili ya Ethiopia mwaka wa 2017 alifanyika kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kuongoza shirika hilo la Umoja wa mataifa lenye makao yake makuu mjini Geneva, Uswizi.

Kiongozi huyo amekuwa akionekana sana kwenye vyombo vya habari hasa baada ya kuzuka kwa janga la virusi vya corona mjini Wuhan, China mwishoni mwa 2019.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, msemaji mmoja wa shirika hilo amesema kuwa haliwezi kutaja majina ya watu wanaonuia kuchukua nafasi hiyo.

Hata hivyo mataifa yote 194 wanachama wa WHO yana hadi Septemba kutuma majina ya watu yanayopendekeza kupitia barua za siri , kwenye bodi ya shirika hilo habla ya uchaguzi kufanyika mwaka ujao.

Wanadiplomasia wameambia Reuters kwamba uungaji mkono wa Tedros kutoka kwa mataifa ya kiafrika ni muhimu ingawa kuna tashwishwi iwapo ataungwa mkono na taifa lake la Ethiopia lililomuidhinisha wakati wa nyuma.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG