Ofisi yake imesema kwamba wafungwa wengine 70 ambao walikamatwa wakati wa maandamano ya kuetea demokrasia nchini humo wataachiliwa huru.
Kati ya walioachiliwa huru ni mwanaharakati wa haki za kiraia Zaki Hannache, ambaye alikamatwa mwezi Februari kwa madai ya kueneza vitendo vya Ugaidi na kusambaza habari za uongo.
Maandamano makubwa yalitokea katika miji kadhaa ya Algeria mapema mwaka 2019, na kumlazimisha aliyekuwa rais wa muda mrefu Abdelaziz Bouteflika kujiuzulu.
Maandamano yaliendelea hata baada ya Abdelmadjid Tebboune kuingia madarakani.
Waandamanaji walimuona Tebboune kama sehemu ya utawala uliokuwepo na ambao haungeleta mabadiliko yoyote.